JOSE MOURINHO
Kocha mpya kwa mara ya pili kuifundisha klabu hiyo inayomilikiwa na tajiri wa kurusi Roman Abrahimovic anatarajiwa kutangaza kikosi ama baadhi ya wachezaji waliopo sasa ambao anatarajia kuendelea nao msimu ujao na wale anaotaka kuwatema pale atakapokutana nao kwa mara ya kwanza July 10…ambapo tayari amewatahadharisha wachezaji watakaokuwa chini yake msimu ujao kwamba wanapaswa kutokuwa wabinafsi kama wanataka mafanikio ya klabu.
. 
Enzi hizo Jose Mourinho akishangilia kwa kunyanyua kombe la ligi kuu England akiwa pamoja na wachezaji wa klabu hiyo wanaodaiwa kuwa maswahiba wake wakubwa nahodha John Terry na kiungo Frank Lampard.
Alikaririwa Mourinho akisema…kuna kauli moja ambayo huwa nawaambia wachezaji kila klabu ninayokwenda,ambapo hata july 10 nitakapokutana nao pia nitawaambia…'kama wewe ni mchezaji wa kulipwa,sio mbinafsi,kama unatanguliza maslahi ya klabu mbele kuliko wewe binafsi,na kama upo hapa kufanya kazi kwa asilimia mia moja kwa kushirikiana na mimi pamoja na wachezaji wenzako,hapo tutakuwa na mahusiano mazuri sana lakini kama wewe ni mbinafsi,haujali mafanikio ya klabu na mashabiki wake kwa hakika tutakuwa katika mahusiano mabaya sana kati yangu mimi na wewe" alisema Mourinho
FERNANDO TORESS
Fernando Toress ni mmoja wa wachezaji ambao hawapo kwenye orodha ya wachezaji watakaofanya naye kazi msimu ujao kwa madai kwamba hakubaliani na uwezo wake klabuni hapo.
ANDRE VILLAS-BOAS
Andre Villas-Boas ni kocha aliyewahi kukinoa kikosi cha chelsea kwa mida mfupi na kisha kutimuliwa na sasa anafanya vizuri Tottenham na kwa sasa anahusishwa na kutakiwa na PSG kwa kitika kikubwa cha pesa
0 comments:
Chapisha Maoni