KAMATI
kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa imeyarudisha
majina yote matatu ya wagombea wanaowania nafasi ya mwenyekiti wa
halmshauri ya wilaya ya Mbinga ambapo imeuwagiza uongozi wa CCM
mkoa wa Ruvuma kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika haraka iwezekanavyo
kabla ya julai mosi mwaka huu.
Akizungumza ofisini
kwake Katibu wa CCM wa mkoa wa Ruvuma Vellena Shumbusho
alisema kuwa majira ya saa za asubuhi amepokea barua toka makao makuu ya
Chama Cha Mapinduzi (DODOMA) ambayo inataarifa ya kuyarudisha
majina matatu ya wagombea.
Katibu
huyo wa mkoa shumbusho aliyataja majina matatu ya walioomba
kugombea nafasi hiyo kuwa ni diwani wa kata ya Kipapa Allanus
Ngahi, Allani Mahai diwani wa kata ya Maguu na Nathaniel Charle
diwani wa kata ya Matili.
Alieleza
kuwa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Taifa baada ya
kusitisha uchaguzi huo katikati ya wiki iliyopita na kuonekana
kuwepo hali mbaya ya kisiasa katika wilaya ya Mbinga ambayo imekuwa
ikiishutumu kamati ya siasa ya mkoa wa Ruvuma kuwa ndio
iliyoshinikiza kukata jina moja la mgombea kwa sasa imaamuru kuyarejesha majina
yote matatu kama walivyoomba wenyewe hapo awali.
Alifafanua
kuwa baada ya ofisi yake kupata tarifa hiyo ya kuyarejesha
majina yote toka kamati kuu ya CCM Taifa imemwagiza Katibu wa Chama Cha
Mapinduzi wa Wilaya ya Mbinga kuhakikisha kuwa anafanya utaratibu
wa kuaandaa mkutano wa uchaguzi kabla ya Julai mosi mwaka huu na si
vinginevyo.
Kwa upande
wake Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mbinga Anastansia Amasi
alipohojiwa kwa njia ya simu alisema kuwa tayari amepokea
taarifa hiyo ya kuyarejesha majina yote ya wagombea na kwamba
uchaguzi unatarajiwa kufanyika kesho ambapo nafasi ya mwenyekiti
madiwani waliogombea ni Allanusi Ngai wa kata ya Kipapa,
Allani mahai wa kata ya Maguu na Nathanieli Charle wa kata ya Matili na
nafasi ya makamu mwenyekiti waliogombea Winfridi Kapinga diwani wa kata
ya Ngima, Prisca Haule na Agness Mahangula ambao wote ni madiwani
wa viti maalumu.
Alibainisha
kuwa awali Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma kilikuwa
kimetangaza nafasi mbili katika halmshauri ya wilaya ya Mbinga
ambazo ni Mwenyekiti na makamu mwenyekiti ambapo katika nafasi ya
mwenyekiti madiwani watatu walijitokeza kuwania nafasi hiyo na nafasi ya makamu
mwenyekiti pia madiwani watatu walijitokeza kuwania nafasi hiyo lakini
kamati ya siasa ya mkoa ilipoketi ilikata jina moja la
mgombea wa nafasi ya mwenyekiti ambalo lilionekana kuleta mtafaruku
mkubwa kwa madiwani wa halmashauri hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni