Home
»
Unlabelled
» HALI YA NELSON MANDELA BADO NI TETE
Rais
mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa hospitalini kwa siku
ya nne ambako anapokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu.
Duru kutoka
kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, zinasema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka
94, yuko katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa.Jamaa zake pamoja
na aliyekuwa mkewe Winnie Madikizela-Mandela, walimtembelea hospitalini
Jumatatu
Mwanawe Mandela Zenani (Mandela-Dlamini), pia alirejea
kutoka nchini Argentina, ambako yeye ni balozi.Serikali imekuwa ikisema
kuwa hali ya Mandle inatia wasiwasi ingawa madaktari wameweza
kuidhibiti.
Amekuwa katika chumba ya
wagonjwa mahututi tangu kulazwa hospitalini Jumamosi kwa mara ya tatu
mwaka huu.Mwezi Disemba , bwana Mandela alilazwa hospitalini kwa siku 18
baada ya kupata maradhi ya mapafu
Kumekuwa na taarifa za simanzi
kwa mara ya kwanza huku familia yake ikikusanyika kando yake, baadhi ya
watu wakisema kuwa ni muda wamwache Mandela aende zake.Bwana Mandela,
mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa
ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu wa duru za
urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya
kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu. Msemaji wa serikali Mac Maharaj
amesema kuwa maafisa katika hospitali wanataka kudhibiti idadi ya watu
wanaozuru hospitali hiyo ili wampunguzie bwana Mandela usumbufu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo
Jumamosi.Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma,
amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba
wakati huu anapougua.
Watu wengi walipata matumani baada ya bintiye
Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata
nafuu.Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini
London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
0 comments:
Chapisha Maoni