Mbunge
wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA, (Kulia), na mbunge
wa Iramba Magharibi, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu
Lameck Nchemba (Kushoto), wakinyoosheana vidole walipokutana mjini
Dodoma kwenye semina ya wabunge kuhusu Ukimwi, iliyoandaliwa na chama
cha wabunge walio katika mapambano dhidi ya UKIMWI (TAPAC), Jumamosi
Juni 22, 2013.
Kisa na mkasa wa hali hiyo ni pale Mchungaji
Msigwa alipofoka kuwa, Mwigulu ndiye injinia wa machafuko kwenye
shughuli za CHADEMA na kwamba ana uchu wa madaraka akitumia neno la
kimombo "POWER HUNGRY", hali iliyopelekea Mwigulu kujibu mapigo kwa
kusema, Mchungaji Msigwa anaweweseka. anayeshuhudia ni Mbunge wa
Nyamagana CHADEMA, Ezekiel Wenje ambaye baadaye aliwaaamua na kuingia
ukumbini. Hata hivyo mambo yaliendelea kuwa hivyo hivyo ndani ya ukumbi,
hadi mama Anne Kilango Malecela alipowatuliza.
|
0 comments:
Chapisha Maoni