WADAU TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII KAMA ITAKUKWAZA LAKINI NDIO UNYAMA WA BINADAMU WA SASA….KUNA WANAOKESHA USIKU KUCHA WAKIMLILIA MUNGU AWAJALIE KUZAA LAKINI WENGINE WANATUPA WATOTO WASIOKUWA NA HATIA…PICHANI NI MAITI YA KITOTO KICHANGA KIKIWA KWENYE MFUKO WA RAMBO.
Wakazi wa eneo la Magomeni zilipovunjwa nyumba za KOTA jijini Dar es salaam leo wakishuhudia mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa umri wa siku moja akiwa ametupwa huku akiwa amekufa katika eneo hilo na mtu asiyefaamika.
Gari la askari polisi wa kituo cha Magomeni usalama wakiwa katika eneo ambalo ametupwa mtoto mchanga akiwa amekufa kwa ajili ya kuchukua mwili wake na kumpeleka sehemu husika.
Maiti ya Kitoto kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri wa siku moja ikiwa imepakiwa kwenye gari la polisi.
Wakazi wa jirani na eneo hilo wakiwa wamekusanyika eneo la tukio.
|
MCHOME BLOG INAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA KICHANGA HIKI NA ALAANIWE ALIYEFANYA UNYAMA HUU.
0 comments:
Chapisha Maoni