Searching...
Jumanne, 4 Juni 2013

AJALI ILIYOUA WATU SITA JANA HUKO MBEYA.


Kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Barakaeli Masaki

HIZI NI BAADHI YA MAITI ZILIZO OKOLEWA PUNDE BAADA YA AJALI KUTOKEA  
MWILI WA DEREVA WA DALADALA ALIYE FARIKI PAPO HAPO UKIPELEKWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI RUFAA MBEYA
******************************

Watu sita wamefariki Dunia na wengine Sita kujeruhiwa katika ajali ya Barabarani iliyo tokea Nane nane Darajani eneo la Uyole Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na madereva mmoja wa Hiace. 

Masaki amesema dereva wa Hiace amefahamika kwa jina la Meshack Hosea aliye kuwa anaendesha Gari nambali T178 AAV aina ya Toyota Hiace inayofanya kazi Sokomatola na Uyole ambapo muda huo ilikuwa ikitokea Sokomatola kuelekea uyole.

Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.

Maiti nne hazijatambuliwa hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria katika Daladala hiyo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.

Aidha amesema majeruhi sita wamelazwa katika hospitali ya Rufaa wakiwemo wanawake watano na Mwanamke mmoja . Ambao mpaka sasa majina yao hayatambuliwa kutokana na kujeruhiwaa vibaya.

Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni  mwendo kasi wa Magari hayo na wito ameutoa kwa Madereva kuwa makini na kufuata sheria za Barabarani ili kuepusha ajali ambazo zingeweza kutokea. Ikizingatiwa hilo ni eneo la Jiji.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!