WATEJA WA VODACOM KUELIMISHWA KUTUMIA M-PESA ILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA
Home
»
Unlabelled
» WATEJA WA VODACOM KUELIMISHWA KUTUMIA M-PESA ILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA
Meneja
Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (kulia)
akielezea kwa waandishi wa habari huduma ya M-pesa benki popote
inayowaunganisha wateja wa Benki ya Amana na nyingine mbalimbali nchini
kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti kwa njia ya M-pesa wakati wa zoezi
la kuwaelimisha wateja wa benki hiyo tawi la Kariakoo jijini Dar es
Salaam leo. Wa pili kushoto ni Kaimu Meneja wa Tawi hilo Khamis Gumbo. Meneja
wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akifafanua
jambo kwa mteja wa Benki ya Amana Tawi la Kariakoo Suleiman Mahmud
kuhusu huduma ya M-pesa Benki popote inayowapa uwezo wateja wa Amana
kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao kwa njia ya M-pesa. Kushoto ni
Meneja Masoko wa Benki ya Amana Fatma Mruma na Kaimu Meneja Tawi la
Kariakoo Khamis Gumbo. Vodacom imeanza kampeni ya kuwaelimisha wateja
namna ya kunufaika na huduma ya M-pesa benki popote inayopatikana kwenye
benki mbalimbali za biashara hapa nchini.
Mteja
wa Benki ya Amana Suleiman Mahmud akielezea namna anavyoifahamu huduma
ya kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti ya Benki hiyo kwa njia ya M-pesa
wakati wa zoezi la kuelimisha wateja kuhusu huduma ya M-pesa benki
popote iliyofanyika katika Tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Wanaomsikiliza ni Meneja wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanznaia
Salum Mwalim (wa kwanza kulia), Meneja Masoko wa Benki ya Amana Fatma
Mruma (wa Kwanza kushoto) na Kaimu Meneja wa Tawi hilo Khamis Gumbo.
0 comments:
Chapisha Maoni