STEVE MC CLAREN AKIWA NA FERGUSON
Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Manchester
united Steve McClaren ameiambia BBC Radio5 kwamba alizungumza siku chache
zilizopita mambo mbalimbali kuhusu klabu ya Manchester lakini Sir Alex
hakuonyesha dalili zozote za hiki kilichotokea sahivi "niliongea
naye siku chache zilizopita,na hakuonyesha dalili zozote za hiki kilichotokea
leo,kwahakika sidhani kama kuna mtu yoyote anayejua sababu ya Ferguson
kujiuzulu mpaka hapo atakapoamua kusema mwenyewe au mtu wa karibu sana na
familia yake…hili ni jambo la kushtukiza na kuhuzunisha sana”alisema bwana Mc
Claren.
AVB AKIWA NA FERGUSON.
Kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas ameiambia Sky Sports kwamba "ni mshtuko mkubwa na
habari za kuhuzunisha kusikia Sir Alex
anastaafu kazi,kwa hakika ligi kuu imempoteza mwalimu bora na mkongwe ambaye
alikua mfano mzuri wa kuigwa na kocha vijana kutokana na mafanikio yake katika
soka…mkongwe ameondoka,nitamkumbuka milele,namshukuru kwa maneno yake ambayo
ameniachia,kwa hakika ni mtu ambaye ninamuheshimu sana”alisema AVB.
BENITEZ NA BABU FEGIE
Kocha wa muda wa Chelsea Rafael
Benitez ameiambia Sky Sports: kwamba
"ninapenda sana kushindana na Sir Alex Ferguson. Ninamtakia kila la kheri na
nimatumaini yangu atafurahia maisha yake nje ya soka”alisema Benitez.
0 comments:
Chapisha Maoni