Searching...
Alhamisi, 23 Mei 2013

RAIS AWAAPISHA MABALOZI WAPYA IKULU JIJINI DSM

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal  na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi  wapya waliopaishwa leo ikulu jijini Dar es Salaam.aliyesimama mbele kushoto no Balozi Liberata Mulamula anayekuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini Marekani.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi mpya wa Tanzania Uholanzi Wilson  Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga,Mwakilishi  wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva Balozi Modest jonathan Mero  na Balozi mpya wa Tanzania katika falme za Kiarabu(UAE)Mbarouk Nassor Mbarouk.Kabla ya uteuzi Balozi Liberata Mulamula alikuwa msaidi wa Rais  Masuala ya kidiplomasia na aliwahi kuwa katibu mkuu wa nchi za  Maziwa  Makuu.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ikulu jijini Dar es Salaam amemwapisha Jaji  Aloycius Mujuluzi kuwa Mwenyekiti wa  tume ya kurekebisha sheria pamoja na mabalozi wanne watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.Mabalozi walioapishwa leo ni pamoja na Balozi mpya katika umoja wa Falme za kiarabu(UAE) Mbarouk Nassor Mbarouk,Balozi mpya wa Tanzania nchini Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga na Mwakilishi wa  kudumu Tanzania Umoja wa mataifa Geneva Balozi Modest Jonathan Mero. 
Picha na Freddy Maro-IKULU

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!