Searching...
Jumanne, 14 Mei 2013

MTU MMOJA ATUPA MAPEPO SHULENI NA KUWAVAA WANAFUNZI NA KUPAGAWA NA KUGALAGALA CHINI.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda maeneo hayo.

Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.

Hapa mtumishi wa mungu aliamua kuingilia kati na kuwaombea wanafunzi hao.
binti mmoja kati ya waliokumbwa na majini hayo akiwa amelala bila kujitambua.
hata hivyo taarifa zaidi zinadai kwamba kuna mtu mmoja alikua anaombewa na mtumishi wa mungu kisha mambo yalipochanganya akapagawa na kukimbia hadi shuleni hapo na kuyatupa majini hayo na kisha kuwavaa wanafunzi.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!