Searching...
Jumatatu, 20 Mei 2013

EXPORT KUFUNGIWA KUNUNUA MAZOA LINDI

LINDI Serikali mkoani Lindi imepitisha azimio  la kuifungia kampuni ya Export trade Ltd (ETC)kufanya biashara ya kununua mazo ya biashara Ufuta na Korosho  mkoani humo.

Azimio hilo limepitishwa na kikao cha ushauri mkoa (RCC)wakati wajumbe walipokuwa wanajadili changamoto zinazo wakabili wakulima wa zao la korosho mkoani humo.


Mwenyekiti wa kikao hicho mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick mwananzila alisema tatizo la soko l  zao la korosho mkoani humo linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinaweza kutatuliwa na wakulima, viongozi wa vyama vya ushirika , na makapuni yanayofanya biashara za kununua mazao hayo.

Mwanazila alisema pamoja na changamoto nyingi zinazokabili soko la korosho mkoani humo lakini pia  makapuni yanayonunua zao hilo yanachangia kuzorotesha mfumo kwa kushindwa kutoa bei ya maslai kwa wakulima wakati huo zikiwa na uwezo mkubwa wa kuwalipa wakulima bei mzuri.

Mkuu huyo alisema kutokana na hai hiyo kampuni ya Export Trading compain (ETC)ndiyo  kinara na chanzo kikubwa cha  migogoro iliyotokea mkoani humo kwa kuwahamasisha wanunuzi wa mazao hayo kununua kwa bei ya chini  ya kuwathulumu wakulima kwa kuwalipa bei ndogo.

Kikao cha ushauri  mkoa Rcc kimepitisha azimio la kampuni ya Export Trading Compain kutopewa kibali cha nunua mazoa ya biashara mkoani humo.


LINDI INAUPUNGUFU WA WALIMU WA SEKO 570
LINDI mkoa wa Lindi unakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu 570 wa madaraja  mbalimbali katika shule zote 115 za sekondari zilizopo mkoani humo kwa sasa.

Hayo yamebainishwa na afisa elimu taaluma kitengo cha elimu ya watu wazima mkoani ;Lindi Friday Sondasi katika mahojiana na radio one mjini Lindi

Kwa sasa mkoa huo una walimu 127 kati ya mahitaji halisi ya walimu 1787 baada ya mkoa huo kupokea walimu wapya 220 kati ya 333 waliopangiwa kufanya kazi mkoani humo mwaka huu ambapo wengine 113 bado hawajaripo hadi sasa,

Sondasi alisema kuwa upungufu huo wa walimu amechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha taaluma na kusababisha  matokeo mabaya ya mitihani ya wanafunzi wa sekondari mkoani humo

Alisema kuwa  kutokana na hali hiyo baadhi ya shule yenye kidato cha kwanza hadi cha nne zimekuwa kiziendeshwa na walimu kati ya wawili hadi wanne tu na hivyo kuwafanya wanafunzi kukosa baadhi ya vipindi vya masomo muhimu.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!