Katibu Tawala Wilaya ya Chunya Sosthenes Mayoka akikabidhi funguo za
vyumba vitatu vya madarasa kwa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi
Mkwajuni Wilayani Chunya baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na Vodacom
Foundation. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya
Mwakifulefule. Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki.
Katibu Tawala Wilaya ya Chunya Sosthenes Mayoka akikabidhi funguo za
vyumba vitatu vya madarasa kwa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi
Mkwajuni Wilayani Chunya baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na Vodacom
Foundation. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya
Mwakifulefule pamoja na wanafunzi wa shule hiyo. Hafla hiyo imefanyika
mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim (katikati)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya
Mwakifulefule (kulia) na Katibu wa Mbunge wa Songwe Agapito Kilongozi
kabla ya kuanza kwa hafla ya makabidhiano ya vyumba vitatu vya madarasa
katika shule ya msingi Mkwajuni Wilayani Chunya mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiwa na
wanafunzi wa darasa la sita wa shule ya msingi Mkwajuni Wilayani Chunya
Jackson Anthon (kulia) na mwenzake Erica Agustino. Wanafunzi hao
walijibu kwa ufasaha maswali ya ufahamu wa huduma za Vodacom ya Cheka
nao na M-pesa wakati wa hafla ya makabidhinao ya vyumba vitatu vya
madarasa vilivyokarabitiwa na Vodacom Foundation. Vodacom Foundation
imeahidi kuwapatia wanafunzi hao vifaa vya shule, sare na vitabu vya
kiada kwa ajili ya darasa la sita na la saba.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkwajuni Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya
wakifuatilia kwa furaha hafla ya makabidhiano ya vyumba vitatu vya
madarasa vilivyofanyiwa ukarabati mkubwa na Vodacom Foundation katika
mikakati yake ya kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini. Hafla
hiyo ilifanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki iliyoongozwa na Katibu
Tawala wa Wilaya ya Chunya Sosthenes Mayoka
0 comments:
Chapisha Maoni