WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA
SAA 09:20HRS HUKO ENEO LA CHAMSALAKA – CHIMALA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA
YA MBARALI MKOA WA MBEYA . GARI T.627 AEA/T T346 AUE AINA YA SCANIA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ABDU S/O OMARI,MIAKA 43,MBENA,MKAZI WA IRINGA LILIMGONGA
MTEMBEA KWA MIGUU MARIAM D/O INCHAGI,MIAKA 18,MUWANJI,MKULIMA MKAZI WA CHIMALA
NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI . MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA CHIMALA MISHENI . DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO
KITUONI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI
WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA
GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA KUSABABISHA
KIFO NA MAJERUH.
MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA
SAA 11:30HRS HUKO ENEO LA NUMBER ONE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE
MKOA WA MBEYA. GARI T.520 BDZ AINA YA TATA MALI YA KAMPUNI YA BONITE BOTTLES
LTD MOSHI LIKIENDESHWA NA DEREVA
AINEA S/O ELIA @ SYANGA,MIAKA 38,MCHAGA,MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MPANDA
PIKIPIKI T.451 CBV AINA YA KING AITWAE
SIKITU S/O ELIA ,MIAKA 38,MSAFWA, MKAZI WA MCHANGANI KIWIRA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO
HAPO NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE
FRED S/O SIGARA,MIAKA 28,MSAFWA,MKULIMA MKAZI WA NDAGA TUKUYU AMBAYE AMELAZWA
KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE . CHANZO NI MWENDO KASI . MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA IGOGWE MISHENI . DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO
KITUONI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI
WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA
SAA 12:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA 1. DEBESHA S/O
ABUSHA,MIAKA 23 NA 2. ADINA S/O
ALABAYO,MIAKA 24 WOTE RAIA WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA
KIBALI . MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO TARATIBU ZINAFANYWA ILI
KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI . KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII
KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA
SHAKA IKIWEMO WAGENI KUTOKA NJE YA NCHI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
[ BARAKAEL MASAKI -
SSP ]
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni