Searching...
Jumatano, 3 Aprili 2013

BREAKING NEWS-MABOMU YARINDIMA NA MPAKA WA TANZANIA NA ZAMBIA WAFUNGWA KUFUATIA VURUGU KATI YA WAISLAMU NA WAKRISTO

Habari za uhakika na za kuaminika zilizotufikia sasa hivi ni kwamba watu kadhaa wamejeruhiwa kufuatia vurugu kubwa ambazo zimezuka hii leo huko TUNDUMA kati ya waislam na wakristo kufuatia kauli ya mkuu wa wilaya ya Momba mkoani Mbeya  bw ABIHUDI SAIDEA ya kuwataka waislam kuendelea kuchinja na kuwazuia wakristo kuchinja na badala yake kula nyama iliyochinjwa na waislam.

Akizungumza na Blog hii shuhuda wa vurugu hizo amesema baada ya vurugu hizo kupamba moto jeshi la polisi imewalazimu kuingilia kati na kupiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao kitendo ambacho kimepelekea baadhi ya watu kujeruhiwa.

Aidha ameongeza kuwa mpaka kati ya Zambia na Tanzania umefungwa kufuatia vurugu hizo na hivyo kusababisha msururu mrefu wa magari kutoka pande zote mbili yaani Tanzania na Zambia

picha za vurugu hizo zitafuata baada ya muda mfupi kutoka sasa.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!