WAFUASI WA RAILA ODINGA WAANDAMANA, WAWILI WAUAWA,ODINGA
AKUBALI,BARAK OBAMA AMPONGEZA KENYATA
Muda mchache baada ya uamuzi wa
majaji hao wafuasi wa waziri mkuu Raila Odinga waliandamana mjini Kisumu,
Magharibi mwa Kenya kupinga uamuzi huo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari
kutoka nchini Kenya taarifa zinasema watu wawili walipata majeraha ya risasi
katika ghasia hizo kwenye eneo hilo analotokea Raila Odinga, aliyewasilisha
mahakamani kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi aliyosema yalikumbwa na
udanganyifu mkubwa.
Kwa upande wake afisa mmoja wa
polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema watu wawili wameuwawa na
wengine 11 wamejeruhiwa katika ghasia hizo. Wakaazi wa eneo la kisumu wanasema
wamekuwa wakisikia milio ya risasi usiku wa kuamkia leo na hadi wakati huu
haijajulikana ni kina nani hasaa waliokuwa wanafyatua risasi hizo.
Wakati huo huo wafuasi wa odinga
wakiandamana kupinga uamuzi huo wa mahakama wafuasi wa rais mteule Uhuru
Kenyatta walimiminika jijini Nairobi wakipiga filimbi, wengine wakipiga honi za
magari huku wengine wakiimba kusherehekea ushindi wa kiongozi wao.
Katika hotuba yake Kenyatta
amewahimiza wakenya kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi na kusema
yuko tayari kufanya kazi na kuwahudumia wakenya wote bila ubaguzi.
Kenyatta mwenye umri wa miaka 51,
alipata zaidi ya kura milioni 6.13, ikilinganishwa na zile za Odinga milioni
5.3. Katika uchaguzi huo wa Machi 4 kulishuhudiwa idadi kubwa ya wapiga kura
katika historia ya nchi Kenya.
Takribani wakenya milioni 14.3
walijisajili kama wapiga kura na zaidi ya kura milioni 12.3 zikapigwa.
Hata hivyo Raila Odinga amekubali
kushindwa na kuwatakia kila la kheri Uhuru Kenyatta na makamu wake mteule
William Ruto wanapojianda kuendesha serikali mpya.
Sasa Uhuru Kenyatta ambaye ni
mwanaye rais wa kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta ataapishwa rasmi
Aprili 9 kama rais wa nne wa Kenya. Kenyatta atakuwa rais wa pili barani Afrika
kukabiliwa na mashtaka katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC.
Rais huyo mteule pamoja na mgombea
wake mwenza William Ruto wote wanakabiliwa na mashtaka kuhusiana na ghasia za
baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008 ambapo zaidi ya watu 1,200 waliuwawa huku
wengine wengi hadi leo wakiachwa bila makao.
Kesi ya Ruto inatarajiwa kuanza
mwezi Mei huku ya Kenyatta ikitarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.
Wakati huo huo Rais wa Marekani
Barrack Obama na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron
Muda mchache baada ya mahakama ya
juu kutoa uamuzi wake wa kumthibitisha Uhuru Kenyatta kama rais halali wa Kenya,
ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, ilitoa taarifa ya kuendelea
kushirikiana na Kenya.
Marekani nayo pia imetoa taarifa ya
kumpongeza Kenyatta huku ikiwahimiza wakenya kudumisha amani katika kipindi
hiki. Marekani pia imesifu ujasiri wa Raila Odinga kwa kukubali na kuheshimu
uamuzi wa koti.
Habari hii ni kwa hisani ya DW.DE
0 comments:
Chapisha Maoni