Searching...
Alhamisi, 5 Septemba 2013

AGUSTINO MREMA ALAMBA MATAPISHI YAKE,AIPIGIA MAGOTI CCM,AMUOMBA PINDA MSAMAHA.

 
AGUSTINO LYATONGA MREMA
NAIBU WAZIRI MKUU MSTAAFU.
Mbunge wa Vunjo mheshimiwa Agustino Lyatonga Mrema leo ametoa kali ya mwaka bungeni baada ya kujiunga na kambi ya CCM na kuwapaka matope wapinzani wenzake hadi kufikia kuwakana huku akimuomba radhi waziri mkuu kwa kitendo alichowahi kukifanya siku za nyuma cha kusaini waraka wa kutokuwa na imani na waziri mkuu.
...Huu ni muendelezo wa story kutoka bungeni leo alhamisi september 05,na kama hukubahatika kuisoma basi iangalie hapa hapa mchome blog ni stori ya 4 zilizopita...
basi baada ya mapambano yliyochukua zaidi ya dakika 30 kati ya askari wa bunge dhidi ya wabunge wa upinzani waliokua wanapinga Mheshimiwa Mbowe kutolewa nje kwa nguvu na askari zaidi ya 40,hatimaye askari walishinda na wabunge wote wa upinzani wa vyama vyote walitoka nje kasoro Mheshimiwa Mrema,ambapo baada ya kubaki peke yake alipewa nafasi ya kuchangia muswada huo ambapo badala ya kuchangia alitumia muda wake wote kukisifia chama cha mapinduzi,kuwaponda wapinzani na kumuangukia waziri mkuu na kumuomba radhi.
Mheshimiwa Mrema alianza kwa kusema..."Nakushukuru sana mheshimiwa naibu spika,kwanza naomba watanzania wajue kwanini jana na leo sijatoka bungeni wakati wenzangu wa upinzani walipoamua kususia bunge...mimi ndio kiongozi wa kituo cha demokrasia hapa nchini ambapo vyama vyote vya siasa ni wanachama,kwahiyo sioni sababu ya kususia viako"..yaani mimi nawashangaa sana hawa wapinzani,kwenye mambo mazuri hawanishirikishi,kwenye mambo mabaya tu ndio wananishirikisha,kipindi nagombea ubunge pale vunjo walisimamisha mgombea wao,kwanini hawakusema sisi ni wapinzani waniache peke yangu nipambane na ccm? sasa leo hii wananiambia nitoke nje,je nikirudi nikikuta mtu kakalia kiti changu hapa nitawaambia nini watu wangu wa vunjo?? hatoki mtu hapa,tutapambana hapa hapa ndani mpaka kieleweke ila nje sitoki ng'ooo!!!!alifunguka naibu waziri mkuu mstaafu Agustino Mrema.
baada ya kuwaponda sana wapinzani akaendelea kumuomba samahani waziri mkuu.
"kwanza naijutia sana nafsi yangu Mheshimiwa waziri mkuu,kwa kitendo changu cha kuwa mmojawapo wa wabunge waliosaini waraka wa kutokuwa na imani na wewe kipindi kile,ninaomba unisamehe mheshimiwa waziri mkuu,naomba unisamehe sana....(ilikua kidogo aseme sitarudia tena,ila hilo hakusema)
 baadae nitaweka video ya sakata zima la bungeni dodoma ili mjionee yale yote yaliyojiri mjengoni.  WASHIRIKA WANGU WA UKWELI.

1 comments:

 
Back to top!