Searching...
Jumapili, 29 Juni 2014

UJUE UWANJA,MWAMUZI NA HISTORIA YA UHOLANZI NA MEXICO KABLA YA MECHI YA LEO

Katika muendelezo wa michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Brazili,leo jumapili June 29 ni hatua ya pili ya 16 bora kutafuta tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo ambapo timu nne zitashuka dimbani usiku wa leo.
TIMU YA TAIFA YA UHOLANZI-2014
Majira ya saa moja kamili za usiku za Afrika mashariki vigogo viwili vya soka duniani Uholanzi na Mexico vitashuka dimbani kumenyana huku majira ya saa tano kamili pia kwa saa za Afrika ya Mashariki vigogo wengine Costa Rica na Ugiriki vitaonyeshana kazi.
TIMU YA TAIFA YA MEXICO-2014
Tukianza na Uholanzi na Mexico timu hizi katika historia ya soka zimewahi kukutana uso kwa uso mara sita ambapo Uholanzi ameshinda mara tatu, Mexico mara mbili na kutoka sare mchezo mmoja, na wote wamefungana magoli 11 kila mmoja.
 
UWANJA WA SOKA WA CASTELAO
 Mechi hii itachezwa katika uwanja huu wa Castelao uliopo katika mji wa Fortaleza,uwanja ambao umejengwa mwaka 1973 na una uwezo wa kuchukua watazamaji 60342 wakiwa wamekaa wote kwenye viti.

PEDRO PROENCA-MWAMUZI WA LEO.
Mechi hii itachezeshwa na mwamuzi wa kati Pedro Proenca,mwamuzi msaidizi namba moja ni Bentino Miranda,mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jose Trigo wote wa Ureno na mwamuzi wa mezani ni Carlos Vera kutoka nchini Ecuador.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!