Timu ya Kilimanjaro Stars imetinga hatua
ya nusu fainali ya michuano ya chalenji, baada ya kuifungashia virago
Uganda kwa mikwaju ya penati. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare
kwa kufungana mabao 2-2 ndani ya dakika 90, huku Uganda wakianza
kuongoza na baadae Mrisho Ngasa kuisawazishia Kilimanjaro na kuongeza
bao la pili lililodumu hadi mapumziko. Uganda walipata bao la
kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare na timu hizo
kwenda katka hatua ya mikwaju. Kilimanjaro
walikosa penati mbili zilizopigwa na Erasto Nyoni na Mbwana Samatta,
huku Uganda nao wakikosa penati mbili. Waliopata penati kwa upande wa
Kilimanjaro ni Amri Kiemba, Athuman Iddi chuji na Kelvin Yondani. Penati
hizo ziliingia hatua ya pili huku Kipa wa Kilimanjaro Ivo Mapunda
akiibeba Tanzania k2a kudaka penati ya hatua pili na kuifanya Tanzania
kutinga katika hatua hiyo ya nusu fainali.
Jumamosi, 7 Desemba 2013
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni