Nkongo, ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya Fifa,
alipigwa na wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Stephano Mwasyika na Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, katika mechi ambayo Azam walishinda 3-1 wakati timu
hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 10 mwaka
jana.
Israel Nkongo wa Dar es Salaam amepangwa
kuchezesha mechi ya Simba na Yanga itakayofanyika katika Uwanja wa
Taifa, Oktoba 20.
Nkongo, ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya Fifa,
alipigwa na wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Stephano Mwasyika na Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, katika mechi ambayo Azam walishinda 3-1 wakati timu
hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 10 mwaka
jana.
Nkongo alipata balaa jingine baada ya kuondolewa
dakika za mwisho kuchezesha mechi ya mwisho wa msimu uliopita kati ya
Simba na Yanga, Mei 18 mwaka huu na mechi hiyo ikachezeshwa na Martin
Sanya wa Morogoro na kushuhudia Yanga ikishinda mabao 2-0.
Kuondolewa kwa Nkongo katika mechi hiyo ya
mwishoni mwa msimu uliopita, kulitokana na ushauri wa ofisa usalama wa
Fifa kushauri kuwa iwapo angechezesha mwamuzi huyo, Yanga wangeweza
kufanya vurugu kutokana na Yanga kudai alivuruga mechi yao dhidi ya
Azam.
Nkongo alisababisha Mwasyika kufungiwa mwaka moja
na kulipa faini ya Sh milioni moja kutokana na kosa hilo huku Jerry
Tegete akisimamishwa kwa miezi sita na wengine kama Cannavaro, Omega
Seme na Nurdin Bakari wakifungiwa mechi tatu na kila mmoja kutozwa faini
ya Sh500,000.
Baada ya kupita vizingiti vyote hivyo, Mwanaspoti
linaweza kuthibitisha kuwa sasa Nkongo atakuwa katikati katika mechi ya
watani itakayopigwa Oktoba 20.
Hata hivyo, haitakuwa ajabu iwapo ofisa usalama wa
Fifa akishauri tena kuwa mwamuzi huyo abadilishwe tena kutokana na
kuhisi kuwa Yanga wanaweza kumkataa.
CHANZO NA MWANASPOTI.
CHANZO NA MWANASPOTI.
0 comments:
Chapisha Maoni