Kwa mujibu wa matokeo ya taarifa ya uchunguzi wa jeshi la polisi nchini kenya shambulio la kigaidi jijini Nairobi,Mwanamke gaidi anayefahamika kwa jina la White Widow, Samantha Lewthwaite, hakuhusika na tukio la shambulio la kigaidi la westgate jijini
Taarifa hiyo inasema kwamba magaidi waliotekeleza shambulio hilo walikua ni wanne tu na sio 15 kama ilivyodhaniwa hapo awali.
Major Emmanuel Chirchir amesema washambuliaji hao kwa majina walikua ni Abu Baara al-Sudani, Omar Nabhan, Khattab al-Kene na Umayr,
jeshi la polisi la kenya limethibitisha kwamba katika shambulio hilo hakukuwa na gaidi mwanamke na kumaliza uvumi kwamba gaidi mkongwe mana mama Lewthwaite alihusika.
Mwana mama huyu mjane mwenye umri wa miaka 29 amekuwa mshukiwa mkuu wa ugaidi baada ya jeshi la Interpol kutangaza kwamba ni mtu hatari sana kwa ugaidi duniani
0 comments:
Chapisha Maoni