Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi
akikagua gwaride la Kikundi cha Kukabiliana na Uhalifu kwa Haraka (Rapid
Response Team) kilichohitimu mafunzo yao katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mwishoni
mwa wiki.
Wahitimu wa RRT wakiapa Kiapo cha Utii
mbele ya Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.
Wahifadhi wakifuatilia kwa makini zoezi
la uhitimishwaji wa mafunzo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Dk.
Christopher Timbuka, John Shemnkunde, Mtango Mtahiko na Godwell Meing’ataki.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA Martin
Loibooki akisoma maelezo kuhusu mafunzo hayo kwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi
akiongea na wahitimu.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA Martin
Loibooki (kulia) akiwa na Kamanda Venance Tossi.
Wahitimu wakionyesha zoezi la
kumsogelea adui wakiwa tayari kwa lolote.
Mashambulizi yanaendelea baada ya adui
kuonekana huku vumbi la risasi likionekana kwa mbali.
Wakufunzi Genes Shayo na Martin Mthembu
wakionyesha wageni waalikwa na wanahabari matundu ya risasi zilizofyatuliwa na
wahitimu.
Picha ya pamoja ya wahitimu na Mgeni
Rasmi.
Makamanda wa Vita dhidi ya Ujangili walioendesha mafunzo haya. Kutoka kulia ni Genes Shayo,
Venance Tossi na mtaalamu kutoka Afrika Kusini Martin Mthembu.
Picha zote na Mdau Pascal Shelutete wa
TANAPA
0 comments:
Chapisha Maoni