RAIS WA ZAMANI WA MISRI-BWANA HOSNI MUBARAK.Helkopta ya jeshi la Misri iliyombeba rais wa zamani wa Misri bwana Hosni Mubarak ikiwa angani kutoka gereza alilokuwemo na kumpeleka moja kwa moja katika hosiptali ya jeshi baada ya kuachiliwa huru kwa masharti ya kukaa nyumbani kwake bila kutoka.
Raia wa Misri wanaomuunga mkono Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak wakisherehekea nje ya mahakama ya Tora jijini Cairo muda mfupi baada ya Mubarak kuachiliwa huru kwa masharti ya kukaa nyumbani kwake bila kutoka.
CAIRO-MISRI
Hosni Mubarak ameondoka kutoka jela ya Tora mjini Cairo kwa helikopta ya
kijeshi na kupelekwa katika hospitali ya kijeshi. Hii inakuja baada ya
mahakama kuamuru achiliwe
Kiongozi huyo atapelekwa kwa hospitali ya kijeshi ambako inaaminika
atapokea matibabu ya maradhi ya moyo iliyoko kaskazini mashariki mwa
Cairo atakakosalia chini ya ulinzi mkali.
Mwendesha mashitaka mkuu wa Misri ametoa idhini rasmi aya kuachiliwa kwa
Mubarak mwenye umri wa miaka 85 kwa kuliagiza gereza hilo kumuachia
huru.
0 comments:
Chapisha Maoni