Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe akiwahutubia wakazi wa Ilula jana. |
Na Gustav Chahe, Kilolo
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na maendeo (CHADEMA)
Freeman Mbowe amesema muarobaini wa matatizo ya nchi na migongano iliyopo ni
serikali tatu.
Aliyasema hayo katika mkutano wa
wazi wa kujadili rasimu ya Katiba mpya uliofanyika katika kiwanja cha Ilula Wilaya
ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa.
Alisema kukiwa na serikali tatu kutakuwa
na utaratibu mzuri wa kunufaika na raslimali za taifa kwa upande wa
Zanzibar na Tanganyika.
Amesema katika suala zima la
Katiba mpya watu wanatakiwa kuacha tofauti zao ili kuweza kujadili mambo yaliyo
ya muhumu tu.
Alisema majadiliano ya rasimu ya
Katiba mpya hayapaswi kufanyika kwa kificho kwa kuwa ni mali ya watanzania
wote.
“Tunapo zungumza suala la katiba
ya nchi yetu tuache dini na tofauti zetu pembeni ili tuweze kutengeneza katiba
nzuri. Watanzania wanastahili kushirikishwa” alisema Mbowe.
Alisema katika taifa kumekuwa na
mmomonyoko mkuwa wa wananchi ambao unasababishwa na baadhi ya watu kujigeuza
kuwa miungu watu.
Alisema lengo la Chadema ni
kutaka kila mmoja aweze kuwa huru na kuwa pamoja kuishi kwa kuheshimiana na
hasa katika imani.
“Tunataka kila mmoja awe na haki
ya kumiliki ardhi badala ya watu wachahe kuhodhi kila kitu. Tumeona kuna kuna
watu wachache wanataka kutengeza katiba inayowalinda wa. Tunapozungumzia
utawala hatumzungumzi kimwete bali tunataka kuweka utawala ambao kila mtu
atakayeingia madarakani aweze kufuata taratibu hizo” alisema.
Kwa katiba tuliyo na ya leo
tunaweza kuwa na rais chizi na tukiwa na rais chizi ataipeleka nchi kichizi
hivyo hivyo na itabidi tukubali tu.
Alisema Katiba mpya itaweza kuwabana
wabunge watakaochaguliwa ili waweze kurudi kuwatumikia wananchi wao badala ya
kuhamia na kuishi Dar es Salaam.
“Watawala wetu siku hizi
wanafanya mambo ya siri. Wanasaini mikataba hya siri, wanauza madini na gesi
kwa siri na kufanya nchi kama ni mali yao.Katiba mpya itayamaliza mambo ya siri
na kila mmoja atajua kinachoendelea” alisema.
Naye mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu
akihutubia katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa katika
Manispaa ya Iringa alisema umefika wakati wa Tanganyika kufufuka kutoka wafu na
kuwa na serikali yake ili kuendesha mambo yanayohusu Tanganyika kwa taratibu
zake bila kuingiliana.
“Rais asiyetaka mabadiliko na
ushauri hafai. Pia waziri ye yote atakayeteuliwa na rais atapigiwa kura bungeni
kupima uwezo wake” alisema Lissu.
0 comments:
Chapisha Maoni