Katika hali ya kutapa tapa Manchester United wameonyesha nia ya kuingilia dili la Chelsea kwa kutaka kumnasa mshambuliaji Samwel Etoo ambaye yupo sokono kwa dau la paundi milioni 5 tu,kutokana na klabu yake ya Anzhi kutaka kupunguza bajeti yao kwa kiwango kikubwa kwa kuwauza wachezaji ghali klabuni hapo.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho yupo katika mikakati mizito ya kusajili mshambuliaji ambapo ameonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo mcameroon ambaye aliwahi kufanya naye kazi kipindi wakiwa Inter Milan.
Gazeti la Italia la Gazzetta Dello Sport limeandika kwamba Manchester United wameingia katika mbio hizo kama njia moja wapo ya kujihami endapo kama mchezaji wao anayeshinikiza kuondoka klabuni hapo Wayne Rooney ataondoka basi wawe na msaidizi wa Robin Van Persie.
Mazungumzo ya Manchester United na wakala wa Etoo yamepangwa kufanyika kesho jumanne huko London japo wachambuzi wa soka wamesema huenda huo ni mchezo wa kuwavuruga Chelsea akili zao ili badala ya kuongeza nguvu kumsajili Rooney basi waelekeze nguvu zao kwa Etoo.
0 comments:
Chapisha Maoni