Baadhi ya washiriki wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba.…
Baadhi ya washiriki wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba.
Baadhi ya wawezeshaji wakijadiliana jambo katika Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba.
Warsha ya wajumbe wa Baraza la Mtandao wa Wanawake na Katiba ikiendelea.
BARAZA la Mtandao wa Wanawake limekutana
lililoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali limekutana kwa siku
mbili kujadili masuala ikiwemo namna ya ushiriki wa wanawake katika
mabaraza yanayojadili rasimu ya Katiba Mpya. Kwa mujibu wa vyanzo wa
habari hizi washiriki hao walikutana kwa siku mbili, yaani Agosti 16 na
17 mwaka huu Makao Makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) eneo la
Mabibo jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa mada zilizowasilishwa na kujadiliwa na wajumbe wa warsha
hiyo ni pamoja na Mchakato wa Katiba Mpya na Ushiriki wa Wanawake
katika Hatua mbalimbali, ikiwemo uchambuzi wa rasimu ya Katiba Mpya
iliyowasilishwa na Diana Kidala wa Jukwaa la Katiba na mada ya Umuhimu
wa Kuwepo kwa Sauti za Wanawake katika Katiba Mpya iliyotolewa na
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya.
Mada zingine zilizowasilishwa na kujadiliwa na wajumbe hao ni pamoja
na Uwasilishaji wa Masuala Muhimu ya Kijinsia yaliyojitokeza katika
rasimu ya Katiba Mpya ya Mkurugenzi Mtendaji wa WFT, Mary Rusimbi na ile
ya Masuala Muhimu ya Wanawake ya Kuiimarishwa na Kuingizwa katika
Katiba Mpya iliyowasilishwa na Vicky Lihiru kutoka ULINGO.
Pamoja na mambo mengine pia wajumbe hao walijenga mikakati ya pamoja
kuendeleza ushiriki wa mtandao katika hatua zinazofuata kwenye mchakato
wa upatikanaji wa Katiba Mpya yenye mrengo wa usawa wa jinsia nchini.
Baraza hilo la wajumbe lilifungwa na Bi. Betty Minde kutoka KWIECO.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
0 comments:
Chapisha Maoni