Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon akiwa na miaka 32 alitua kwenye klabu hiyo ya Urusi tangu mwaka 2011 akitokea Inter Milan ambapo alikua chini ya kocha Mreno Jose Mourinho ambaye anataka kuendelea naye sasa Chelsea.
Chelsea ni moja ya vilabu vikubwa ulaya vinavyofuatilia mwenendo wa kisoka wa msukuma ndinga huyo wa Cameroon Samwel Etoo Phils japo wakala wake anaonyesha dalili za mchezaji wake kutua Napol.
Akizungumza kwa kinywa chake mwenyewe leo asubuhi Etoo amesema "nimefanya kazi na makocha wengi na wakubwa sana Duniani,lakini ni mmoja tu na si mwingine ni Jose Mourinho,ni yeye tu.
"ni mmoja kati ya makocha bora duniani, na nimekua na mafanikio makubwa nilipata mafanikio makubwa sana nikiwa naye pale Inter Milan.ninatamani kufanya kazi na yeye tena kwasababu hauwezi kuboreka ukiwa naye...hakika ni kocha mzuri"I alisema Etoo.
Enzi hizo Jose Mourinho akiwa na timu ya Inter Milan hapa akilinyanyua kombe la klabu binga ulaya mwaka 2010 ambapo Etoo alichangia kwa kiasi kikubwa kufikia mafanikio hayo.
Wakati Etoo akiwakaribisha Chelsea,wakala wake amesema "Hamu na ndoto yake kwa Italia ni kuvaa jezi ya Napoli,japo mpaka sasahivi hatujapata ofa kutoka kwao"alisema wakala wa Etoo.
Timu ya Chelsea imekua ikihaha kutafuta mshambuliaji tangu arejee klabuni hapo Jose Mourinho ambapo wamekua akipambana kumsajili Wayne Rooney,ambapo hadi sasa timu hiyo imegonga ukuta mara mbili baada ya ofa zao kukataliwa na Manchester United huku wakisisitiza kwamba mchezaji wao hauzwi lakini Chelsea wapo mbioni kutuma ofa ya tatu kabla dirisha la usajili halijafungwa tarehe0 2.092013.
0 comments:
Chapisha Maoni