Searching...
Alhamisi, 22 Agosti 2013

KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA KESHO KUHITIMISHA MAJADILIANO YA KATIBA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo.
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kinatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Agosti 24 na 25, 2013 mjini Dodoma Chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete.
    Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitakachofanyika Agosti 23,2013 mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye, maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambacho kimeketi kwa Siku tatu kuanzia Agosti 20, 21 na leo 22, 2013 mjini Dodoma.
 Kwa mujibu wa Ndugu Nape, Ajenda Kuu ya kikao cha NEC ni kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mchakato wa chama Kama Baraza la Katiba la kitaasisi  kukamilisha mjumuisho wa mchango na maoni yake Tayari kuwasilisha kwa Tume ya Katiba.
         Ndugu Nape alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kujadili na kutoa maoni yao kuanzia ngazi ya Chini ya mashina na Matawi.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!