Searching...
Alhamisi, 22 Agosti 2013

BREAKING NEWSSSSSSSS!!!!! WATU 7 WANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA NDEGE MANYARA,NDEGE YAENDELEA KUELEA ZIWANI


5H-TZU, 1997 Cessna 208B C/N 208B0639, Tanzanair Caravan NDEGE YA TANZANAIR PICHA KUTOKA MAKTABA
Habari ambazo zimeifikia MCHOME BLOG muda mfupi uliopita zinasema watu saba ambao waliokua wakisafiri na ndege ndogo ya kampuni ya TANZANAIR wamenusurika kufa baada ya ndege hiyo waliyokua wakisafiria kutoka Bukoba kuelekea Jijini Dar es salaam kupitia Zanzibar kuzima injini moja ikiwa angani maeneo ya anga la Manyara na rubani wa ndege hiyo kufanya ujasiri mkubwa kwa kuishusha ndege hiyo ziwa manyara na kuokoa maisha yake pamoja na abiria wake sita.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema baada ya Ndege hiyo kutua ziwani walipata misuko suko lakini watu waliwahi kuwaokoa na sasa wamekimbizwa katika hosiptali ya rufaa ya Seliani Jijini Arusha kwaajili ya matibabu japo taarifa zinasema wote wapo salama kwani ni abiria watatu tu kati yao waliopata michubuko ya hapa na pale kufuatia mikiki mikiki ya ziwani manyara,hata hivyo taarifa zinaarifu kwamba hadi muda huu ndege hiyo inaelea ziwa manyara huku jitihada za kuondolewa ziwani hapo zikiendelea.
Hata Hivyo mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Manyara amekataa kuzungumzia ajali hiyo kwa madai kwamba mwenye jukumu la kuizungumzia ajali hiyo ni kamanda wa polisi mkoani Arusha ambapo hata hivyo simu ya kamanda Liberatus Sabasi iliita pasipo majibu japokuwa alikua katika eneo la tukio.
Mwanahabari wetu alipofika hosiptalini walipo majeruhi hao walikatazwa kuwapiga picha na taarifa zinaeleza kwamba abiria hao ni wanasheria ila haijajulikana walikua wanakwenda Dar es salaam kwa shughuli gani.
Picha za ajali hii kule ziwa manyara zitakujieni muda sio mrefu endeleeni kutembelea MCHOME BLOG kwa habari za uhakika.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!