Msemaji
Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari
MAELEZO Bw. Assah Mwambene jijini Dar es Salaam alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara
hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa News
for Rwanda na wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda
Juvenal Havyarimana.
“Taarifa hizi hazina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema
Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha
na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo
na ukweli wowote.
Madai
hayo yaliandikwa jana na mitandao ya Rwanda wakidai kuwa mama
Salma Kikwete ni Mnyarwanda na ni binamu wa aliyekuwa rais
wa zamani wa Rwanda.
Wakati huo
huo, wadadisi wa mambo wa kimataifa wameonesha kushangazwa na hatua ya
makusidi ya Wanyarwanda ya kujaribu kumpakazia Rais Kikwete na Mkewe
Mama Salma Kikwete, Mmakonde wa Lindi, kwa kumzushia mambo ya ajabu na
kushangaa zaidi kuona mitandao hiyo ya udaku ya Rwanda haijaonesha jinsi
Rais Kagame alivyovurumishiwa mawe na Wanyarwanda wenzake alipokuwa
Chuo Kikuu ya Oxford nchini Uingereza.
"Unajua
ustaarabu wa Watanzania ni wa hali ya juu ndio maana mitandao yake
iliamua kuacha kuripoti habari za kutukanwa na kupigwa mawe Rais Kagame
na Wanyarwanda wenzake wanaomchukia (angalia video) alipotembelea Chuo
Kikuu cha Oxford hivi karibuni", amesema mdadisi mmoja wa Uingereza,
James Parker wa North London.
Mdadisi
mwingine wa Uingereza, Bw. Mark Sutton, amesema hiyo ni moja ya njia
chafu za Wanyarwanda katika kujaribu kulipiza kisasi kwa kutimuliwa
maelfu ya ndugu zao waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini
Tanzania, na sasa wanahaha wapi kwa kuwaweka kwenye ka-nchi hako kadogo
ka Afrika Mashariki.
"Kutimuliwa
kwa Wanyarwanda nchini Tanzania kutaleta vituko vingi sana, na hii ya
kumsingizia Mama Salma Kikwete kuwa anahusiana nao ni mojawapo - mengi
yatakuja na Watanzania wasishangae maana Wanyarwanda wametaharuki na
hawajui wafanyeje kwa kupokea zaidi ya wenzao 10,000 waliokuwa wakiishi
kinyume cha sheria nchini Tanzania," amesema mdadisi mwingine, Adam
Hayes.
0 comments:
Chapisha Maoni