MHESHIMIWA PETER SERUKAMBA.
Wabunge 13 wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa kamati ya miundombinu wamenusurika kuungua moto baada ya gari walilokua wakisafiria kuwaka moto wakiwa katika shughuli za kutembelea miradi mbalimbali ukiwemo uwanja wa kimataifa wa ndege huko bukoba mkoani Kagera.

akizungumza na MCHOME BLOG mwenyekiti wa kamati hiyo mheshimiwa Peter Joseph Serukamba amesema ajali hiyo ilitokea ghafla na kuona moshi mwingi sana ukijaa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Costa ambayo walikodishiwa kwaajili ya shughuli hiyo.
Aidha Mheshimiwa Serukamba amesema wabunge wote walitoka salama na hakuna yeyote aliyejeruhiwa ila tu wengine walilazimika kutokea madirishani baada ya mlango wa gari hilo kuwa mdogo ghafla!!! ..."yah nikweli hali ilikua mbaya ghafla maana iliwalazimu waheshimiwa wengine kutokea madirishani kutokana na mlango kuwa mdogo,ila wote tupo salama na tumechukua gari lingine na sasa tunaendelea na safari yetu kama ilivyopangwa" alisema mheshimiwa Serukamba.
0 comments:
Chapisha Maoni