Marehemu Margaret Thatcher.
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher amefariki dunia.
Thatcher alikuwa na umri wa miaka 87 na msemaji wake ameelezea kuwa alifariki kutokana na ugonjwa wa kiharusiThatcher alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu wa Uingereza na anasemekana alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mageuzi makubwa ya kisiasa nchini Uingereza tangu alipochukua mamlaka mwaka 1979.
Pia Margaret Thatcher alisifika sana kuwa mwanamke mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Uingereza.
MUNGU AILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU-AMINA.
Habari kwa hisani ya BBC-Swahili.
Habari kwa hisani ya BBC-Swahili.
0 comments:
Chapisha Maoni