Searching...
Jumamosi, 30 Machi 2013

Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro
Mkuu wa wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro amewataka wananchi  wa Makete  kushiriki katika  ukarabati wa miundombinu ya barabara pindi tatizo linapotokea hasa maeneo korofi


Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu kwa njia ya simu Bi.Matiro alisema wananchi wanatakiwa kuwa na ushirikiano pindi barabara zinapokuwa zimeharibika ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Makete 


 


Hata hivyo alisema kuwa viongozi wa Tanrods mkoa wa Njombe wameshapewa taarifa kuhusiana na tatizo hilo lililoko katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo hasa katika kijiji cha Ivalalila ambapo magari ya kutoka Mbeya kuja Makete yanashindwa kupita kulingana na ubovu wa barabara hiyo

Mtandao huu ulifika eneo la tukio nakujionea hali halisi  ya barabara ambapo mpaka sasa hakuna mawasiliano kutoka Makete kwenda jijini Mbeya kupitia Ivalalila kutokana na shimo lililopo eneo la Ivalalila.

  Mtandao huu haukiishia hapo ulikwenda moja kwa moja kuongea na wamiliki wa vyombo vya usari ambapo mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Japanise, Junich Daniel alimarufu kama  Mwarabu alisema "kwa hali hii inakoelekea usafiri wa Makete na Mbeya hautakuwepo kutokana na tunaingia gharama nyingi kufanya marekebisho ya magari kutokana na mara nyingi kugongesha katika mashimo ya barabarani"

Akiendelea Mwarabu alisema"natumia fursa hii kumuomba mbunge na uongozi mzima bila kumsahau waziri mwenye dhamana ya ujenzi kuweza kutufanyia marekebisho katika barabara za wilaya ya Makete kuwa hali tete hususani nyakati za masika 


Na EDWIN MOSHI,Makete

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!