Searching...
Jumamosi, 20 Julai 2013

MAAJABUUUU NA KWELI.....MOURINHO KUREJEA INTER MILAN BAADA YA MIAKA 3 CHELSEA.


Mourinho 'will quit Chelsea for Inter in three years'
JOSE MOURINHO-KOCHA CHELSEA.
Raisi wa Inter Milan Massimo Moratti ameanika wazi kwamba aliyewahi kuwa kocha wa Inter mreno Jose Mourinho alimuambia ataondoka Chelsea baada ya miaka mitatu ya kuitumikia Chelsea na kurejea ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A.
Mourinho ameweka historia Inter kwa kuwawezesha kushinda taji au kombe la ligi na klabu bingwa ulayakwa kipindi cha miaka miwili aliyoifundisha timu hiyo baada ya kuondoka Chelsea mwaka 2007.
Baada ya hapo Mourinho alitua Hispania na kuifundisha kwa mafanikio makubwa klabu kongwe na tajiri ya  Real Madrid kabla ya kubwaga manyanga na kurejea nyumbani Chelsea kunako Stamford Bridge msimu huu ambapo sasa anaendelea na mikakati na vita ya kutafuta wachezaji bora wa kukiimarisha kikosi chake cha Chelsea.
Inter Milan's club president Massimo Moratti (L) and manager JosMOURINHO AKIFURAHIA JAMBO NA RAISI WA INTER MORATTI.
‘Nilimpigia simu Mourinho kumtakia mafanikio katika klabu yake ya zamani ya Chelsea,’ Moratti aliliambia gazeti la Italia la La Stampa.
‘Alichoniambia,amesema tutakutana tena Inter baada ya miaka mitatu.’
Mourinho aliwahi kukiri kutoka moyoni kwamba vilabu viwili vya Inter na Chelsea ni vilabu ambavyo vipo moyoni mwake daima.
Hata hivyo kocha huyo Mreno mwenye miaka 50 sasa tayari ametia saini ya kuifundisha klabu hiyo ya Chelsea kwa kipindi cha miaka minne kwa maana hiyo ili aweze kurejea Inter ndani ya miaka mitatu ijayo atalazimika kuvunja mkata na Chelsea....na taarifa zaidi zinasema hadi sasa Mourinho anaendelea kumiliki nyumba yake huko jijini Milan nchini Italia aliyokuwa akiishi kipindi akiifundisha klabu hiyo ya Italia

1 comments:

  1. huuuuuuuuu!!!! nilidhani anaukatisha sahivi ningekufa...i like Mourinyo

    JibuFuta

 
Back to top!