Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza
na ujumbe wa Shirika la Misaada la Hanns Seidel Foundation masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na shirika hilo. Wapili
kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Dk. Peter Witterauf,
anayefuata ni Mkuu wa shirika hilo, Kanda ya Afrika, Klaus Liepert, na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo nchini Tanzania, Konrad Teichert.
Viongozi wa Shirika hilo lenye Makao Makuu yake jijini Munich nchini
Ujerumani walimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake, jijini Dar es
Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipokea
zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Misaada la Hanns
Seidel Foundation, Dk. Peter Witterauf. Kulia ni Mkuu wa shirika hilo,
Kanda ya Afrika, Klaus Liepert. Viongozi wa Shirika hilo kutoka Makao
Makuu, Kanda ya Afrika pamoja na Mwakilishi Mkazi wa shirika hilo nchini
walimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake jijini Dar es Salaam
kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na
shirika hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa pili kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Misaada la Hanns
Seidel Foundation. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Dk.
Peter Witterauf, wa pili kulia ni Mkuu wa shirika hilo, Kanda ya Afrika,
Klaus Liepert. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo nchini,
Konrad Teichert na kulia ni Naibu Kamishina wa Polisi Makao Makuu,
Tathimini na Ufuatiliaji, (DCP) Omar Rashid. Viongozi wa Shirika hilo
lenye Makao Makuu yake jijini Munich nchini Ujerumani walimtembelea
Waziri Nchimbi ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kujadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na Shirika hilo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani.
0 comments:
Chapisha Maoni