|
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Dk. Fenella Mukangara akitia saini katika mpira wakati wa hafla ya
uzinduzi wa mashindano ya mpira wa Miguu ya Amani na Umoja Super Cup jijini Dar
es Salaam jana. Mashindano hayo yanaratibiwa na Kikundi cha vijana cha Mambo
Safi kilichopo Kimara Baruti chini ya udhamini wa waziri Mukangara ambapo
jumla ya timu 32 kutoka jimbo la Ubungo zinashiriki mashindano hayo.
|
|
Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akisalimiana na baadhi ya
wachezaji wa timu zinazoshiriki mashindano ya Amani na Umoja Super Cup wakati
alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es
Salaam.
|
|
Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akipiga mpira ikiwa ni
ishara ya kufungua rasmi mashindano ya Amani na Umoja Super Cup wakati
alipokuwa mgeni rasmio katika uzinduzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es
Salaam.
|
|
Wachezaji wa timu
ya Florida FC ambao ni washiriki wa mashindano hayo wakiwa katika picha
ya pamoja kabla ya mechi ya ufunguzi mashindano ya Amani na Umoja Super Cup
yaliyozinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara.
|
|
Wachezaji wa timu
ya Kimara United ambao ni washiriki wa mashindano hayo wakiwa katika
picha ya pamoja kabla ya mechi ya ufunguzi mashindano ya Amani na Umoja Super
Cup yaliyozinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara.
|
|
Wachezaji wa timu
za Florida FC na Kimara United wakigombania mpira wakati wa mechi ya
ufunguzi wa mashindano ya Amani na Umoja Super Cup yaliyozinduliwa rasmi jana
jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk.
Fenella Mukangara. Katika mechi hiyo Kimara United ili ibuka kidedea kwa
kuinyuka Florida FC jumla ya mabao 2 - 0 ambapo magoli yote ya United
yalifungwa na Mshambuliaji Abdallah Mashauri wakati goli la kufutia machozi la
Florida FC liliwekwa kimiani na William Haule.
|
|
Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akipokea risala kutoka kwa
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Amani na Umoja Super Cup Bwana Laurent
Mtoi alipokuwa mgeni rasmi wa hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo jana jijini
Dar es Salaam.
|
|
Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akisalimiana na mashabiki
waliofurika uwanja wa Kimara Baruti kushuhudia uzinduzi wa mashindano ya
mpira wa Miguu ya Amani na Umoja Super Cup jijini Dar es Salaam jana.
Mashindano hayo yanaratibiwa na Kikundi cha vijana cha Mambo Safi kilichopo
Kimara Baruti chini ya udhamini wa waziri Mukangara ambapo jumla ya timu
32 kutoka jimbo la Ubungo zinashiriki mashindano hayo.
|
(Picha Zote na Frank Shija)
0 comments:
Chapisha Maoni