RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko makubwa ya makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wa wizara zote ambapo miongoni mwao kuna wapya na wengine wa zamani wameachwa ambapo sababu kubwa ni kuimarisha utendaji katika nafasi zao.
Akitangaza mabadiliko hayo katibu mkuu kiongozi Bw.Ombeni Sefue amesema makatibu wote walioachwa watapangiwa majukumu mengine.
Walioachwa ni pamoja na katibu mkuu wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Bw.Seti Kamuhanda,aliyekua katibu mkuu maendeleo ya jamii jinsia na watoto Kijazi Mtengwa na mhandisi Omar Chambo aliyekua uchukuzi,ambapo aliyekua wizara ya ardhi Patric Rutabazibwa ameamua kustaafu.kuhusu hatma ya ya david Jairo na Blandina Nyoni amesema bado uchunguzi wao unaendelea.
Sura mpya katika mabadiliko hayo ni pamoja na katibu mtendaji wa tume ya vyuo vikuu Profesa Sifuni Mchome ambaye sasa anakuwa katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi,ambapo katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Peniel Lymo amehamishiwa ofisi ya Rais Ikulu kama naibu mtendaji mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza idara ya mageuzi ya kilimo
0 comments:
Chapisha Maoni