Na Bryceson Mathias
Kutokana
na Matukio ya Uovu, Kashikashi, Karaha Vitisho na Usumbufu wanaoupata
Wananchi kuhusu kuchangia mbio za Mwenge, wanasiasa wenye mtazamo chanya
wanaona Mwenge Uzimwe ukawekwe Makumbusho ya Taifa.
Kauli
za Mwenge uzimwe na kuwekwa Makumbusho ya Taifa, zinatokana na
viashiria vingi vya uovu vinavyotokana na mwenge huo unapokimbizwa
vijijini na Mijini ambapo wananchi na wanasiasa walio wengi wanadai umepoteza lengo lililokusudiwa na waasisi wake.
Watanzania
waliotoa mawazo wanadai, Manyanyaso, kukosekana kwa Haki, Vitisho,
kukosekana Amani na Afya miongoni mwa Jamii dhidi ya Viongozi katika
Mitaa, Vitongoji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mikoa na Taifa kwa sehemu kubwa
mbio za Mwenge zinachangia.
Baadhi
ya Viongozi mijini na vijijini wenye mapenzi mema na wananchi nchini,
wametoa siri wakidai kipindi cha Mwenge kikifika, Wananchi wanakuwa na
Mzigo mkubwa kwa sababu wanalazimishwa kutoa michango mingi kufanikisha
mbio hizo.
Ijapokuwa
wananchi wenyewe wanakuwa hawana hata mulo mmoja, lakini cha kushangaza
wamekuwa wakitakiwa kuchangia Sh. 5,000/- hadi 10,000/-, na walalahoi
wanaposhindwa basi wamekuwa wakilundikwa Lupango na wengine
kunyang;anyway biashara zao ndogondogo.
Kutokana
na kwamba nyakati hizo huwa ni nyakati za kuzindua Miradi mbalimbali,
huwa kuna michango mingi inayoadaiwa ni ya Maendeleo ya kumalizia Miradi
ambapo wananchi hukumbana na adhaa ambazo hufanywa na Watendaji wa
Vijiji na Kata na kuwaacha Maskini.
Mbali
ya Manyanyaso na Kero za michango inayowapelekea watu kufungwa,
Maambukizi ya Magonjwa (Ukimwi) yamekuwa kichocheo kikubwa miongoni mwa
Vijiji na Miji, ambapo Serikali huigharimu kutokana na uharibifu wa
wanafunzi na Jamii.
Kwa
msingi huo, Serikali kwa upande wake, huonekana kama inaangamiza nguvu
kazi yake, na kwamba inapoamuru mwenge ukimbizwe, inatafsiriwa inapeleka
maangamizo kwa watu wake, ingawa lengo ni kupeleka maendeleo, lakini
uharibifu unakuwa Mkubwa zaidi ya tija.
Kingine
kinacholalamikiwa na wananchi na viongozi wa Ngazi chini kuhusu Mbio za
Mwenge, ni matumizi mabovu ya michango inayochangwa na wananchi, kwamba
imekuwa ikiwasomesha na kuwalisha kama si kuwavisha watoto wa watendaji
wa Vijiji Kata Tarafa Majimbo, Wilaya na Mikoa.
Ushahidi wa Vielelezo vinavyotolewa ni kwamba, Idadi ya fedha zinazochangishwa kila Kaya kimaandishi
huoneshwa wachache, lakini kimsingi wanaochangishwa huwa ni wengi ila
taarifa za kiasi kinachopatikana zinachakachuliwa. Inahojiwa fedha hizo
zinakwenda wapi?
Wakati
mwenge mkoani Dodoma (shule ya Msingi Ipagala), kulizunduliwa Matundu
mawili ya ya Vyoo vilivyokarabatiwa, lakini shule hiyo ina wanafunzi
wanakaa chini. Gharama iliyofanikisha uzinduzi huo inatosha kutengeneza
madawati ya shule nzima. je tunafikiri?
Agosti
19, Dodoama; Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk.
Wilbroard Slaa aliulizwa kwenye Rasimu ya mabadiliko Katiba mpya, ni
pamoja na Mbio za Mwenge kuondolewa maana hazina tija zaidi ya kuleta
madhara ya ajali na maambukizi.
Dk.
Slaa katika ufafanuzi wake alisema, kusudi lilolokusudiwa na Waasisi wa
Mbio hizo, limekiukwa badala yake Mbio hizo imekuwa mitaji na vyanzo
vya Ufisadi na kuwanufaisha watu wachache ambapo alisema, Mwenge
unatakiwa Uzimwe na Ukawekwe kwenye Makumbusho ya Taifa, jambo
lililoshangiliwa na wananchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dodoma hivi karibuni, Kaimu Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Dodoma, Susan Kaganda, alisema Watu tisa wamejeruhiwa katika
ajali ya gari kwenye msafara wa mbio za Mwenge.
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308
0 comments:
Chapisha Maoni