Searching...
Jumatatu, 19 Agosti 2013

MKUTANO WA BARAZA LA KATIBA WAFUNGULIWA LEO JIJINI DSM


 katibu mkuu ofisi ya makamu wa rais, bw Sazi salula akizungumza katika mkutano wa baraza la katiba la ofisi ya makamu wa rais jijini dar leo..
 Waziri wa nchi ofisi Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano wa baraza la lakatiba la ofisi ya makamu wa rais jijini dar es Salaam leo.
katikati katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais bw. Sazi Salula, naibu katibu Mkuuu Bw. Ngosi mwihava kulia na kushoto Mkurugenzi wa Idara ya Muungano ofisi ya makamu wa Rais bw. Baraka Baraka katika mkutano wa baraza la katiba la ofisi hiyo jijini dar es salaam leo. (Picha na Evelyn Mkokoi wa ofisi ya makau wa Rais).
Watumishi wa ofisi ya makamu wa rais na baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC wakimsikiliza waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano, hayupo pichani alipofungua mkutano wa baraza la katiba la ofisi ya makamu wa rais jijini dar leo.
........................
Evelyn Mkokoi na Lilian Kisasa
Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa, ameiomba serikali na baraza la katiba kujadili suala la haki za wanawake katika kupatiwa nafasi za juu za uongozi  Serikalini.  Waziri Huvisa ameeleza hay oleo katika mkutano wa baraza la katiba la Ofisi ya makamu wa rais jijini Dar es salaam.
Waziri Huvisa  amesema kuwa, masuala ya jenda ni muhimu kujadiliwa katika nafasi za uongozi serikalini , hasa katika ngazi za juu za uongozi , hivyo amependekeza kuwa katita rasimu ya katikba, wanawake wapate moja ya tatu ya uongozi wa juu katika Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Awali akifungua mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano  Mh. Samia Suluhu Hassan, amewaomba wajumbe wa baraza la katiba la Ofisi ya Makamu wa Rais, wawe Makini , wastahimilivu na wenye hekima na busara katika kuboresha Rasimu hiyo ya Katiba mpya na hatimaye kupata katiba nzuri  kwa watanzania wote . Mh. Suluhu aliyaeleza  wajumbe  wa baraza hilo kuwa majadiliano hayo ya Rasimu ya Katiba Mpya yasiwe ya Kubomoa bali yawe ya kujenga na kuimarisha jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri  Suluhu, amefafanua kuwa mchakato huu wa kutoa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya ulianza kwa kutungwa sheria ya mabadiliko ya katiba yaliyopitishwa na Bunge la jamuhuri la muungano wa Tanzania mwezi November 2011 na kufanyiwa marekebisho mwezi februari 2012 ambapo, sheria hiyo imeainisha hatua  zitazofuatwa  katika upatikanaji wa Katiba ambapo alifafanua kwamba hatua ya kwanza ni kukusanya maoni ya wananchi , hatua ya pili ni kuitisha mabaraza ya katiba , hatua ya tatu ni kuitishwa kwa bunge maalum la katiba , na hatua ya nne ni kura ya maoni ikifuatiwa na kupatikana kwa katiba mpya.
Mheshimiwa Suluhu aliongeza kwa kusema kuwa kuwa tume hiyo ya katiba, imepewa miezi kumi na nane(18) tangu mwezi  mei  2012 kukamilisha kazi yake, hivyo kwa umuhimu huu wa katiba kwa taifa la Tanzania Ofisi ya Makamu ya Rais imeunda baraza la katiba ambalo kwa mujibu wa muongozo wa katiba linatakiwa kujadili na kutoa maoni kwa kuhusisha malengo na majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais amabayo ni Muungano na uhifadhi wa Mazingira , hivyo amewahimiza wajumbe kutoa maoni kwani hawatabanwa na kifungu wala ibara yoyote.
Kwa upande mwingine mheshiwa Suluhu ameipongeza Tume ya mabadiliko ya katiba kwa kazi nzito iliyofanywa ikiwa ni pamoja na kuandika Rasimu ya katiba ambayo wengi wameweza kuisoma na kuielewa.
HABARI NA MICHUZI JR.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!