Searching...
Jumatano, 21 Agosti 2013

DALA DALA DAR ES SALAAM HAZIHESHIMU ALAMA ZA BARABARANI,ZINAWAONEA WATEMBEA KWA MIGUU

 Hapa ni basi la abiria maarufu kama dala dala likipita kwa mwendo kasi huku watu wengi wakisubiri kuvuka (Hawaonekani wapo upande wa pili) katika kivuko cha njia panda ya ITV mwenge jijini DSM
Hapa ni muonekano kama vile hakuna magari barabarani  lakini yapo (hayaonekani) ila ni heshima na utii wa kuheshimu alama za barabarani znzofanywa na magari madogo ya watu binafsi tofauti na daladala
 Kwa makusudi kabisa picha mbili hapo juu zikilionyesha basi hilo la abiria maarufu kama daladala likipita kwa spidi bila kujali wavuka kwa miguu kwenye kivuko chao,lakini kwa heshima angalia hilo gari dogo hapo chini likiwaheshimu wavukaji wawili waliodharauliwa na daladala.
 Baada ya kuwaruhusu akaendelea na safari yake safiiii,hata hajapungukiwa na kitu chochote zaidi ya kutii heshima na kuziheshimu alama za barabarani.
 Hapa pamoja na kwamba hakuna wavuka barabara lakini gari hili dogo linapita kwa mwendo mdogo kwa tahadhari tofauti kabisa na daladala
 Huyu dada alikoswa koswa kugongwa na hilo daladala katika harakati za kuvuka barabara katika kivuko cha wavukaji
Angalia huu utii wa sheria barabarani unaoonyeshwa na magari madogo,utadhani kuna askari wa barabarani kumbe walaa,ni ustarabu tu.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!