Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, leo
Agosti 26, 2013 mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kabla ya
Mwenyekiti wa CCm Rais Jakaya Kikwete (kushoto) kufungua kikao cha NEC,
Agosti 26, 2013
Baadhi ya wajumbe wa NEC, ukumbini. Kulia mstari wa mbele ni Mjumbe wa
Kamati ya Ushauri ya Viongozi wastaafu wa CCM, John Malecela ambaye ni
mwalikwa kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Katibu wa NEC,
Uchumi na Fedha, Zakiah Meghji kabla ya kikao cha NEC kuanza, Makao
Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Mjumbe wa NEC, Dk. Fenela Mkangala na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakijadili jambo kabla ya kikao cha
NEC kuanza leo Agosti 26, 2013, Makamo Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Wajumbe wa NEC kutoka Pemba wakiwa nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza.
Kutoka Kushoto ni Hamadi Bakari Ali, Mwinyi Fakih Hassan, Ali Issa Ali,
Masoud Mohammed Abdallah, Seif Shaaban Mohammed na Mussa Fumu Mussa.
.............................................
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala
mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua
uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa
Kiembesamaki.
Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf
Himid ni pamoja na:-
1.Kushindwa
kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2.Kushindwa
kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.
3.Kuikana
Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma
dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)
imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa
kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor
Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.
Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU
WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013
0 comments:
Chapisha Maoni