Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki akiangalia pembe zilizokamatwa JESHI la polisi mkoani Ruvuma kwa mara nyingine jeshi la polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata nyara za serikali katika wilaya ya Tunduru tukio ambalo limetokea Julai 21 mwaka huu majira ya saa 11:40 alfajiri lililotanguliwa na tukio jingine lililotokea Juni 26 mwaka huu ambapo jumla ya meno....... 18 ya tembo yalikamatwa wilayani humo kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na idara ya wanyamapori pamoja na wananchi wanaotoa taarifa za siri kwa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amesema kuwa sik hiyo ya tukio askari polisi waliokuwa doria walifanya upekuzi kwenye mabasi yaliyokuwa yakianza safari alfajiri katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Tunduru ambapo katika basi moja lenye namba za usajili T315ABS aina ya Scania mali ya kampuni ya WAHIDA walifanikiwa kukamata sanduku moja likiwa na nguo pamoja na vipande 21 vya meno ya tembo
Amesema kuwa vipande hivyo vya meno ya tembo vilikuwa na
uzito wa kilogramu 34.45 na thamani yake ikiwa ni dola za kimarekani 189,475
sawa na fedha za kitanzania shilingi 30,316,000na mkia mmoja wa tembo na
walipoendelea kufuatilia katika mizigo hiyo walibaini kuwepo kwa tiketi moja ya
kusafiria abiria ikiwa na namba
zilizofutwafutwa na walipofuatilia kwenye kitabu cha tiketi waligundua kuwa
tiketi hiyo ilikuwa imesajiliwa kwa jina moja tu.
Na askari walipoendelea kufuatilia ilionekana abiria mwenye
tiketi hiyo na mizigo hiyo iliyotiliwa mashaka aliamua kuitelekeza mizigo yake baada
ya kuwaona askari polisi wakiwa kwenye upekuzi wa mabasi na hivyo mtu huyo
hakuweza kufahamika na jitihada za polisi kwa kushirikiana na wananchi za
kumtafuta zinaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani .
Aidha kamanda Nsimeki ameendelea kuwaomba wananchi na raia
wema kuendelea kutoa ushirikiano mwema kwa jeshi la polisi katika harakati za
kuzuia biashara hiyo haramu inayoendelea kuhujumu uchumi wa taifa.
Katika tukio jingine lililotokea katika kijiji cha Langiro
wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kamanda
Nsimeki amesema tukio hilo lililotokea Julai 22 mwaka huu majira ya saa 7 usiku
ambapo mtu mmoja aliyejulikana kwa jina
la Peter Kapinga(19) aliuawa baada ya kupigwa na mti kichwani na watuhumiwa wa
tukio hilo ni Ingo Kapinga na Elias Kapinga ambapo chanzo niugomvi uliotokea
kwenye disko na ugomvi wao huo ulisababisha kifo kwa sababu ya wivu wa
kimapenzi ulioanzia kwenye muziki huo amba baada ya tukio hilo mtuhumiwa mmoja
Inigo Kapinga alitoroka na mwenzake Elias Kapinga(14) alikamtwa na anahojiwa na
polisikuhusina na tukio hilo.
Habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com
0 comments:
Chapisha Maoni