DC wa Kishapu Bw.Nkhambaku akifanya usafi bila kujali hadhi yake na kuwaonyesha maofisa wa wilaya mfano wa kutoka ofisini na kwenda mtaani kufanya kazi kwa vitendo badala ya kung'ang'ania ofisini.
Hapa mkuu wa Wilaya ya kishapu anavaa vifaa vya kujikinga na uchafu ili aanze kazi.
Mwandishi wa Habari wa SRAR TV bwana Shabban Alley akifanya mahojiano na mkuu wa wilaya ya kishapu wakati zoezi la usafi likiendelea
Baada ya shughuli ya kusafisha kwa
vitendo mkuu wa wilaya alianza kutoa elimu kaya kwa kaya kuhusu umuhimu wa
utunzaji na usafi wa mazingira.
Baada ya uhamasishaji hapa Mwenyekiti wa kitongoji cha mwasele bwana Fedrick Machibya elimu ikamuingia na yeye kuanza kazi ya usafi
DC akizungumza na wamiliki na mafundi wa gereji bubu ambapo amewataka kuiondoa gereji hiyo barabarani.

Baada
ya usafi huo,mkuu wa wilaya alipata muda wa kuzungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara ambapo walizungumza mambo mengi ya maendeleo kuhusu wilaya hiyo.
Wananchi
na waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa wilaya
0 comments:
Chapisha Maoni