Searching...
Jumapili, 15 Septemba 2013

SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI MATATANI,TANZANIA YAENDELEA KUTENGWA.

 
Katika hali inayoonyesha wazi muelekeo wa kuvunjika kwa shirikisho la afrika mashariki kama sio Tanzania kujitoa,umezidi kuonekana baada ya nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kukutana jijini Kigali nchini Rwanda jana katika mkutano waliojadili mpango wa kuwa na visa moja ya utalii ifikapo mwaka 2014 kati ya nchi hizo tatu miongoni mwa nchi wanachama wa shirikisho la afrika mashariki huku wakizitenga Tanzania na Burundi katika mkutano huo,kwa maana kwamba mpango huo hauwahusu Tanzania wala Burundi.
Lakini pia mkutano huo ulizungumzia ama kujadili uwezekano hizo nchi tatu kutumia vitambulisho vyao vya kupigia kura badala ya Passport pale wananchi wao watakapokuwa wanaingia nchi moja kati ya hizo tatu yaani Kenya, Uganda na Rwanda kitendo ambacho wachambuzi wa mambo ya kisiasa wamekitafsiri kama anguko la shirikisho la afrika mashariki.
Mkutano mwingine kati ya nchi hizo tatu unatarajiwa kukaa miezi miwili ijayo jijini Kigali kuona wamefikia wapi katika maazimio ya mipango hiyo miwili mikubwa ya kihistoria kabla ya kufikia makubaliano rasmi.
SWALI NI JEEEE,HAPA INGEKUWA WEWE NDIO RAIS WA TANZANIA AU BURUNDI UNGECHUKUA MAAMUZI GANI????

1 comments:

  1. mi ningeachana nao na kujali mwendelezo wanchi yangu
    kitu nnachoshangaa ni kwa nini Tz inakawia kujitoa... kwani Tz yafaidika vipi na huo ushirikiano? to me its crap and time wastage

    JibuFuta

 
Back to top!