Penny,Lulu na Wema enzi za mahusiano yao.
Mtangazaji nyota nchini ambaye ni mchumba
wa kupika na kupakua wa mwanamuziki Diamond Penny amevunja ukimya na
kutoa onyo kali kwa wasanii wa kike na wasio wasanii kumkalia mbali baby
boy wake Diamond.
Habari za uhakika kutoka kwa mtu wa karibu na Penny anayeishi nae maeneo ya Mwananyamala ambaye pia aliomba hifadhi ya jina lake alisema “ Jamani Penny amejipanga kuolewa na Diamond kwani sasa hivi amecharuka na kutoa onyo kali kwa mwanamke yeyote atakaye msogelea mchumba wake huyo la sivyo ataloga mtu” Alisema dada huyo ambae anafanyakazi nyumba ya jirani na anapoishi Penny
Penny amepiga mkwara huo hasa akimlenga zaidi msanii Lulu na Linah nk huku akitahadharisha kuwa anawaomba wote wenye tabia ya kuchukua wanaume za watu kwani yeye katika maisha yake hajawahi kuchukua mume wa mtu hivyo kama akihisi kuna ajenda yoyote ya siri kati ya mchumba wake na wasanii hao hakika ataloga mtu kwani yeye ni mtoto wa kidigo halisi kutoka Tanga.
Aidha chanzo hicho kiliongeza kusema kuwa penzi la Penny na Diamond limefikia pazuri kiasi cha familia zao kutembeleana na kula pamoja kama wakwe. Hata hivyo ilielezwa kuwa Familia ya Diamond imeshampa Baraka zote mtoto wao ili amuoe kabisa Penny na huku nae Penny akihimizwa kudumisha upendo wa dhati kwa Diamond ambaye tangu aanze kuishi na mtangazaji huyo Diamond amebadilika sana kitabia na hata kiafya....kilifunguka chanzo cha habari hii

0 comments:
Chapisha Maoni