Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA) Bw. Stephen Ngatunga wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mkutano wa Kimataifa wa Wakala wa Forodha katika nchi za Afrika na Mashariki ya kati (RAME 2013) utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Juni 19. Kushoto ni Mkurugenzi mshauri wa TAFFA.
Rais
wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania
(TAFFA) Bw. Stephen Ngatunga akisisitiza kuhusu serikali kulifanyia kazi
suala uundaji wa mkakati wa kutangaza bandari zetu nje ya nchi kwa
kufungua ofisi katika nchi zinazotuzunguka kwa lengo la kuongeza
watumiaji wa bandari . Kushoto ni Mkurugenzi mshauri wa TAFFA na Bw.
Jimmy Mwalugerwa (Mkurugenzi TAFFA).
Viongozi wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA). Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
======= ======= ========
Imeelezwa
kuwa Tanzania itanufaika zaidi kibiashara kupitia bandari ya Dar es
salaam, Mtwara na Tanga kutokana na serikali kuamua kufanya
maboresho makubwa katika sekta ya usafiri wa Bandari na reli.
Hayo
yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Rais wa Chama cha Wakala wa
Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA) Bw. Stephen
Ngatunga wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mkutano wa Kimataifa wa Wakala
wa Forodha katika nchi za Afrika na Mashariki ya kati (RAME 2013)
utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Juni 19.
Amesema
Tanzania kupitia Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena
Tanzania (TAFFA) itakuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaowashirikisha
mawakala 300 wa makampuni ya usafirishaji na upokeaji wa mizigo ,
wafanyabiashara, maafisa wa serikali na mabalozi mbalimbali kutoka nchi
za Mashariki ya kati.
Amesema
mkutano huo wa siku 3 utakuwa na manufaa makubwa kwa wafanyabishara
kutoka Tanzania kujenga mahusiano na kunufaika na fursa mbalimbali
zilizo katika eneo zima la Afrika na Mashariki ya kati ,kuitangaza
Bandari ya Dar es salaam, Tanga na Mtwara pamoja na kukuza utalii
nchini.
Amefafanua
kuwa Tanzania kupitia TAFFA inakuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana
na pendekezo lililopitishwa katika mkutano mkuu wa dunia wa mwaka 2012
uliofanyika mjini Los Angeles, Marekani.
Ameongeza kuwa
katika mkutano huo wa Juni 19, rais wa Shirikisho la Kimataifa la
Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena (FIATA) Bw. Stanley Lim
pamoja na wajumbe waandamizi wa shirikisho hilo kutoka nchi
wanazoziwakilisha watajadili mambo mbalimbali ya kuboresha biashara
katika ukanda wa nchi za Afrika na Mashariki ya Kati (RAME).
Katika
hatua nyingine Bw. Ngatunga amefafanua kuwa maboresho yanayoendelea
hususan katika bandari ya Dar es salaam yanaifanya Tanzania kuwa katika
nafasi nzuri ya kupanua wigo wa kunufaika na ongezeko la fursa za
biashara kwa nchi zisizo na ukanda wa bahari zikiwemo Burundi, Rwanda ,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Zambia na Malawi kuendelea
kutumia usafiri wa reli na Bandari za Tanzania kusafirisha mizigo.
Amesema
kitendo cha serikali kufanya maboresho makubwa ya kiutendaji katika
bandari na reli kimesaidia kuendelea kuleta imani kwa wafanyabishara
kutoka nchi mbalimbali zisizo za ukanda wa Bahari kupitisha mizigo yao
na kuongeza kuwa matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakikwamisha uondoshaji
wa shehena bandarini yamefanyiwa kazi.
Ameeleza
kuwa serikali kukubali kulifanyia kazi suala la ukusanyaji wa mapato ya
Bandari na kuagiza lifanyike kupitia benki badala ya utaratibu wa
awali wa kulipa fedha moja kwa moja bandarini limepunguza urasimu na
kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato katika sekta hiyo.
“Kwanza
suala la ukusanyaji wa mapato bandarini lilisababisha usumbufu mkubwa,
waziri wa uchukuzi alivyoingia tulimweleza na tukamwomba alifanyie kazi
na jambo hilo likatekelezwa sambamba na uboreshaji wa huduma za usafiri
wa reli ili kupunguza mrundikano wa makontena bandarini kanma
ilivyoainishwa katika bajeti ya uchukuzi ya 2013/2014 limetufariji sana”
ameeleza Bw.Ngatunga.
Aidha
ameiomba serikali kulifanyia kazi suala uundaji wa mkakati wa kutangaza
bandari zetu nje ya nchi kwa kufungua ofisi katika nchi zinazotuzunguka
kwa lengo la kuongeza watumiaji wa bandari na kukabiliana na ushindani
pamoja na kuwachulia hatua za kisheria wale wote watakaokwamisha ufanisi
wa shughuli za bandari nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni