Kaimu
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mghulu akizungumza na
wanahabari leo hii, amesema upelelezi huo umezingatia matukio
mbalimbali ya uhalifu yaliyofanyika hapa nchini.
Kuhusu
kumwagiwa tindikali kada wa CCM bwana Musa Tesha, katika kampeni za
uchaguzi mdogo wa Iguga mwezi Septemba mwaka 2011, tayari watuhumiwa
wawili wamekwisha kufikishwa mahakamani na upelelezi upo katika hatua za
mwisho. Endapo watabainika watuhumiwa wengine, nao watafikishwa
mahakamani kwa muda muafaka.
0 comments:
Chapisha Maoni