Searching...
Jumatatu, 9 Desemba 2013

RAIS KIKWETE AHUTUBIA TAIFA SIKUKUU YA UHURU,AWAPIGA VIJEMBE WATU WANAOTAKA KUONGOZA ILI WALIPIZE VISASI

Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Uhuru kwa maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika hivi punde.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa sasa amewasili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuongoza maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika uliopatikana Desemba 9, 1961.
 Upiganajia haki na usawa kwa kila mwananchi wa Afrika Kusini dhidi ya makaburu kwa kipindi hicho, ni miongoni mwa matendo mema atakayozidi kukumbukwa nayo rais mstaafu wa Afrika kusini marehemu Mzee Nelson Mandela
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru yaliyofanyika kitaifa hii leo katika uwanja wa uhuru jijini Dar esa Salaam
Rais Kikwete amesema marehemu mzee Mandela alikuwa ni kiongozi wa pekee aliyepigania maslahi ya waafrika hasa weusi bila kujali kuhatarisha uhai wake, na ikumbukwe kuwa wakati anapigania kuondoa ubaguzi wa rangi, alikuwa akifanya katika mazingira magumu kwa kuwa ukatili na utesaji wa waafrika weusi ulikuwa kwa kiwango cha hali ya juu
"Lakini mzee Mandela alikuwa amekubali kujitoa muhanga, alipambana na ukatili huo bila woga, kama ni kufa wacha nife lakini sitaogopa kuwatetea waafrika, kwa kweli ndugu zangu tumempoteza kiongozi shujaa wa kweli aliyepambana na makaburu bila woga" alisema Kikwete
Amesema kitendo cha kiungwana alichokifanya marehemu Mzee Mandela baada ya kutoka jela cha kuwasamehe wale wote waliomtesa na hata kumfunga jela ni cha kipekee na kina funzo kubwa kwa wananchi na viongozi wote duniani, akimaanisha hakuna haja ya kulipisha kisasi
"Tupo watu hapa tuliopanga kulipiza kisasi, nikipata watanikoma, kiukweli kisasi hakisaidii tujifunze kupitia kwa Mzee Mandela, hakulipiza kisasi, na sisi tusilipize kisasi" alisema Rais Kikwete
Ucheshi na upendo aliokuwa nao Mzee Mandela kwa dunia, ni dhahiri kuwa viongzoi wote wa mataifa makubwa na hata madogo yatafika Afrika Kusini kumzika marehemu Mzee Mandela anayetarajiwa kuzikwa Jumapili Desema 15 mwaka huu huko nchini Afrika kusini

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!