WAYNE ROONEY.
Klabu ya Manchester United imethibitisha kwamba mshambuliaji wake anayewindwa na klabu ya Chelsea
Wayne Rooney ameondolewa katika msafara wa kuelekea nchini Sweden katika maandalizi ya msimu ujao kutokana na maumivu ya bega.
Mshambuliaji wa kimataifa wa England Wayne Rooney alitarajiwa kurejea dimbani akiwa na timu yake katika mchezo wa kirafiki dhidi ya AIK
Stockholm kesho usiku lakini kutokana na maumivu hayo ya bega,lakini wachambuzi wa maswala ya soka wamesema inawezekana sio kwamba Rooney anaumia kila wakati ila ni mzozo kati yake na kocha wake na shinikizo la kutaka kuondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Chelsea.
Hii ni picha iliyokuwa inatumiwa na klabu hiyo ya Manchester United kutangaza mechi hiyo ya kesho huko jijini Stockholm nchini Sweden lakini sasa kutokana na maumivu hayo ya mshambuliaji huyo atakosa mechi hiyo na huenda ikawa doa kubwa kwa mashabiki wa Sweden.
Hata hivyo kocha David Moyes amesema hakuna tatizo kubwa kwa Rooney zaidi ya swala la kitabibu
‘Wayne Rooney ameumia bega lake katika mchezo wa jumamosi’alisema Moyes ‘sio maumivu makubwa na sitarajii kwamba atakuwa nje kwa muda mrefu,ninasikitika sana kwamba anakosa mchezo wa kesho maana tulimtarajia sana kucheza mchezo huu
0 comments:
Chapisha Maoni