Searching...
Jumatano, 15 Januari 2014

TETESI ZA UHAMISHO WA DIRISHA DOGO ULAYA HIZI HAPA.

 JULIAN DRAXLER.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anataka kumsajili mchezaji nyota wa Schalke Julian Draxler, 20, kwa kitita cha paundi milioni 35 kama mchezaji mbadala wa nyota wao waliyemuuza Manchester United Robin van Persie. 
 PAUL POGBA.
Mpango wa Manchester United wa kumrejesha kiungo wao waliyemuuza Juventus Paul Pogba unaonekana kukwama katika usajili wa dirisha dogo japokuwa bado wanayo matumaini ya kumsajili mwishoni mwa msimu huu lakini Pogba amewaambia marafiki zake wa karibu kwamba hana mpangon wa kurejea Old Trafford kutokana na kile alichodai ugumu wa maisha aliowahi kukumbana nao alipokuwa klabuni hapo.
Fernando is being watched by Liverpool

FERNANDO.
Timu ya Liverpool imeingia katika vita kubwa ya kumuwania kiungo wa timu ya Porto Fernando, 26.Timu zingine zinazopigania saini ya kiungo huyo ni Manchester United na Everton.
 CHARLIE ADAM.
Timu ya Galatasaray ya Uturuki inataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Stoke City Charlie Adam, 28, kwa kitita cha paundi milioni 5.
 
  ROMAN ABRAMOVICH.
Tajiri wa Chelsea Roman Abramovich ameonyesha dhahiri imani yake kwa kocha wa timu yake mreno Jose Mourinho kwa kumpa madaraka ya kuamua kuwapa mkataba mpya au kuwauza wakongwe watatu wa timu hiyo Frank Lampard, John Terry na Ashley Cole.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!